Kwa mara ya kwanza Nahodha na Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Argentina Lionel Andrés Messi amefichua ukweli wa kilichomuondoa FC Barcelona na kutimkia PSG ya Ufaransa.
Messi aliihama FC Barcelona mwanzoni mwa msimu huu, huku ukweli wa kuondoka kwake ulifanywa kuwa siri katika kvuli cha kumalizika kwa mkataba wake ndani ya Barca.
Mshambuliaji huyo amefuchua ukweli huo, alipohojiwa na CNN, ambapo amesema: “Nilikuwa nimerudi Hispania baada ya michuano ya Copa America Julai, nilichokuwa nakiwaza ni kwamba mkataba huo uliwekwa pembeni kwa sababu saini yangu tu ndio ilikuwa inasubiriwa kumbe sivyo.”
“Nilipowasili Barcelona niliambiwa hilo la kusaini mkataba mpya haliwezekani tena, hivyo nitafute klabu nyingine kwa sababu hawawezi kuniongezea mkataba.”
“Hilo lilinipa wakati mgumu sana nikaanza kufikiria mengi ikiwamo kubadilisha mfumo wa familia yangu kuacha makazi na kwenda kuanza upya sehemu nyingine.”
“Kujiunga na PSG sikukosea, kilichonisaidia mimi kutulia baada ya kujiunga na PSG ni sura ninazozifahamu hapo na kuzingatia kwamba kuna wachezaji wengi wanaoongea lugha ya Kihispania kama ‘Ney’ ‘Lea’ (Paredes), ‘Fideo’ (Di Maria),” alisema Messi ambaye hadi sasa ameifungia bao moja tu PSG tangu ajiunge nayo kipindi cha majira ya joto.”
Messi ameondoka FC Barcelona huku akiacha kumbukumbu ya kufunga mabao 474 katika michezo 52 aliyocheza tangu mwaka 2004 hadi 2021.
Ametwaa mataji ya Ligi ya Hispania ‘La Liga’ mara 10 msimu wa 2004–05, 2005–06, 2008–09, 2009–10, 2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015–16, 2017–18 na 2018–19.
Kombe la Mfalme ‘Copa del Rey’ mara 7, msimu wa 2008–09, 2011–12, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18 na 2020–21.
Taji la kufungua msimu ‘Supercopa de España’ mara 8 mwaka 2005, 2006, 2009, 2010, 2011, 2013, 2016 na 2018.
Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ‘UEFA Champions League’ mara 4 msimu wa 2005–06, 2008–09, 2010–11 na 2014–15.
UEFA Super Cup mara 3 mwaka 2009, 2011 na 2015
Kombe la Ligi ya Mabingwa Duniani ‘FIFA Club World’ mara 3 mwaka 2009, 2011 na 2015.