Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi amekiri kuwa alijua Neymar wa PSG atajiunga na Real Madrid wakati wa dirisha la usajili lililopita baada ya kuona Barcelona watashindwa kumsajili.

Messi amesema hayo alipokuwa akihojiwa katika Kituo cha RAC1, ambapo aliongeza kuwa Neymar alionesha nia ya kuondoka Paris na nikajua Rais wa Madrid, Florentino Perez na uongozi wa timu hiyo watamfuata kumsajili.

Mambo mengine ambayo alizungumza kwenye mahojiano hayo ni pamoja na uwezo wa kocha wa Manchester City ambao ulisaidia kukuza kiwango chake.

“Nimepata bahati ya kukutana na matukio mengi makubwa mazuri, bado kipindi cha Guardiola nilikuwa mmoja wa wachezaji bora.

“Kila mwaka nimekuwa nikipambana kuongeza ubora, nafikiri ni wakati wa (Pep) Guardiola, ndipo nilipokua sana kisoka wakati huo.”alisema Messi.

Pia mchezaji huyo hakusita kubainisha nyakati mbaya kuwahi kukutana nazo kwenye maisha yake ya mpira, bao lake bora, mechi bora na timu bora pamoja na safu ngumu ya ulinzi kuwahi kukutana nayo.

“Mwaka 2013 na 2014. Nilipata majeraha kwa miezi miwili au mitatu nilikuwa nje.

“Lile nililofunga Rome kwa kichwa na likatupa ubingwa wa Ulaya.

“Ni timu ya taifa ya Hispania tulipocheza nao mechi ya kirafiki kabla ya Kombe la Dunia 2010.Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid tuliyoshinda 2-0. Ilikuwa ya kipekee na msimu huo wa 2010/11 ilikuwa dhidi ya Madrid ya Jose Mourinho.

“Niwe mkweli, kuna wakati nilitaka kuondoka, tatizo halikuwa Barcelona bali kwingine na niliona kama sitendewi haki kwa jinsi walivyokuwa wakini chukulia.alisema Messi

Steve Nyerere, Baraka The Prince wawajia juu wanaovujisha video za faragha
Vijana watakiwa kutumia michezo kudumisha amani na mshikamano