Nyota wa Barcelona Lionel Messi ametwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu barani Ulaya baada ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye ligi zote barani Ulaya msimu uliopita.

Mabao 37 aliyofunga kwenye La Liga msimu wa 2016/17 yametosha kumpa kiatu hicho mfungaji wa muda wote wa Barcelona. Messi sasa ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya nne.

Messi amewahi kutwaa tuzo hiyo katika miaka ya 2010, 2012 na 2013. Baada ya leo sasa Messi amefikia rekodi ya Ronaldo ambaye naye ametwaa tuzo hiyo mara nne katika miaka ya 2008, 2011, 2014 na 2015.

Nyota huyo alifunga mabao hayo kwenye michezo 34 na kumshinda mshambuliaji wa Sporting CP Bas Dost, ambaye alifunga mabao 34 pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund ambaye alifunga mabao 31.

Video: Dkt. Shika akosa mpinzani Lugumi, IGP awaonya wanasiasa
Kenyatta amualika Raila sherehe za kuapishwa, Raila apanga yake