Nahodha na mshambuliaji wa FC Lionel Messi anaongoza kwenye orodha ya wanasoka wanapata mkwanaj mrefu duniani, kwa mujibu wa Jarida la Forbes.

Malipo ya mshambuliaji huyo kutoka nchini Argentina, yanamfanya kuwa mwanandinga anaelipwa pesa nyingi kuliko wachezaji wengine, akimuacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu Cristiano Ronaldo, anaeshika nafasi ya pili kwenye orodha iliyotolewa na Jarida la Forbes.

Uchunguzi uliofanywa na Jarida hilo umebaini kuwa, Messi anakusanya kiasi cha dola za kimarekani milioni 126 (sawa na Pauni milioni 97.2) kwa mwaka, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa kujikusanyia dola milioni 117 (sawa na pauni milioni 90.3) kwa mwaka.

Washambuliaji wa mabingwa wa Ufaransa PSG, Neymar na Kylian Mbappe wanafuatia katika nafasi ya tatu na ya nne.

Orodha kamili ya wanasoka wanakusanya pesa nyingi kwa mwaka, kwa mujibu wa Jariba la Forbes.

  1. Lionel Messi (Barcelona na Argentina) $126m (£97.2m)
  2. Cristiano Ronaldo (Juventus na Ureno) $117m (£90.3m)
  3. Neymar (Paris St-Germain na Brazil) $96m (£74.1m)
  4. Kylian Mbappe (Paris St-Germain na Ufaransa) $42m (£32.4m)
  5. Mohamed Salah (Liverpool na Misri) $37m (£28.5m)
  6. Paul Pogba (Manchester United and Ufaransa) $34m (£26.2m)
  7. Antoine Griezmann (Barcelona na Ufaransa) $33m (£25.5m)
  8. Gareth Bale (Real Madrid na Wales) $29m (£22.4m)
  9. Robert Lewandowski (Bayern Munich na Poland) $28m (£21.6m)
  10. David de Gea (Manchester United na Hispania) £27m (£20.8m)

TANZIA: Mgombea ubunge afariki dunia
Michael Sarpong aivulia kofia VPL