Mshambiliaji hatari wa FC Barcelona, Lionel Messi atashtakiwa na mahakama ya nchini Hispania, kufuatia tuhuma za kukwepa kodi inayokadiriwa kufika dola million 4 za kimarekani.

Jaji mmoja nchini Hispania, ameagiza mshambuliaji huyo, kufunguliwa mashataka kufuatia tuhuma zinazomkabili ambazo zimechukuliwa kama wizi dhidi ya mamlaka ya ushuru nchini humo.

Jaji huyo amesema Lionel Messi alishirikiana na baba yake mzazi aitwake Jorge, hivyo itawalazimu wote wawili kufikisha mahakamani kujibu tuhuma za kushindwa kulipa kodi, itokanayo na malipo ya haki zake za mauzo huko Belize na Uruguay.

Baba mzazi wa Lionel Messi (Jorge Messi)

Hata hivyo Jaji huyo amekataa ombi la kiongozi wa mashtaka, ambaye alitaka baba wa mshambuliaji huyo kusimamishwa kizimbani pekee yake, kutokana na kusimamia masuala ya fedha za mwanawe.

Miaka miwili iliyopita wakati mashtaka hayo yalipofunguliwa, Messi na baba yake walilipa dola milioni tano kwa mamlaka ya kodi nchini Hispania.

Iwapo Messi na baba yake watabainika walikwepa kodi, watakabiliwa na kifungo cha miezi 22 jela.

Utata Vifaa Vya ‘BVR’ Vilivyokamatwa Vikiandikisha Wafanyakazi Dar
Siri Ya Urafiki Wa Mrema Na Magufuli Hii Hapa