Mchawi wa Barcelona, Lionel Messi ameonekana mtulivu kwenye mazoezi ya jana akijiandaa na mechi ya UEFA Super Cup.
Siku chache zilizopita, Messi alicheza dhidi ya AS Roma katika mechi ya kirafiki dhidi ya AS Roma ya Italia, lakini ndani ya uwanja kulikuwa na cheche za aina yake.
Messi alimpiga kichwa na kumkaba koo beki wa Roma, Mapou Yanga-M’Biwa, Barcelona ikishinda 3-0 Camp Nou.
Muargentina huyo hakuoneshwa kadi nyekundu kwa kufanya tukio hilo.



