Mlinda Lango wa Young Africans, Metacha Mnata amevuruga mambo klabuni hapo na sasa amewekwa kando ya kikosi kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Inaelezwa Mlinda Lango huyo ameingia kwenye utata wa kinidhamu baada ya kushindwa kurejea kambini kwa wakati akitokea kambi ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ilipocheza ugenini dhidi ya Algeria.

Taarifa kutoka ndani ya Young Africans ni kwamba Metacha hakufaya mawasiliano yoyote akiwa nje ya kikosi hicho na alianza kuwatafuta viongozi wa benchi la ufundi wakati Young Africans ikiwa ugenini ilipopoteza dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-1.

“Alipowatafuta viongozi ili arudi, tumeambiwa kocha (Miguel Gamondi), alizuia asirejee kwanza akichukizwa na kitu alichokifanya cha kukaa kimya huku wengine waliokuwa naye kwenye timu hiyo ya taifa wakiwa wamerudi,” amesema mmoja wa viongozi wa timu hiyo

“Hatujajua amechukuliwa hatua gani, lakini kwenye timu ilikuwa bado hajarudishwa nadhani kuna mawasiliano anayafanya na viongozi kwanza.”

Mbali na Metacha inaelezwa pia kiungo Jonas Mkude, naye mapema alifanya kosa kama hilo ingawa alijiwahi na kujisalimisha na kupewa adhabu za ndani na baadae kusamehewa.

Benki zawekeza kwenye Dawa hatari za Kichina
Fedha za Kigeni: Wafanyabiashara msitumie madalali - BoT