Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya TAMISEMI, Dkt. Grace Magembe amesema kuwa anashukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya na kuipa kipaumbele katika maswala ya lishe,afya tiba, afya kinga na eneo la mama na mtoto.

Dkt. Magembe amebainisha hayo leo wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA), unaongozwa na kauli mbiu “Kuimarisha uchanjaji wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 miongoni mwa Madaktari Wanawake Tanzania”.


“Sisi kama Madaktari Wanawake Tanzania tunajukumu kubwa la kutoa elimu kwa jamii kwa maana ya kubadilisha fikra potofu na kuwafikishia huduma bora wananchi”, amesisitiza Dkt. Magembe

Naye Rais wa MEWATA Dkt. Mary Charles ameeleza lengo kuu la mkutano huo kuwa ni kuhamasisha Madaktari Wanawake kuwa mabalozi kwa wananchi juu ya kupata chanjo ya Uviko 19.

Dkt. Mary amesema kuwa pia mkutano huo unalenga kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Tanzania, kongo kuandaa mkutano wa wafanyabiashara
DC akanusha kuibwa viungo vya marehemu