Wakati kikosi cha Kagera Sugar kikitarajiwa kuhama kambi kutoka Kagera kwenda Uganda kocha wa timu hiyo, Mecky Maxime amesema anauona mwanga kwa vijana wake.

Kagera Sugar ni miongoni mwa timu 16 zenye ushindani mkali katika Ligi ya Tanzania Bara msimu uliopita haikufanya vizuri kama ilivyozoeleka ikimaliza nafasi ya 11 na alama 35 kibindoni.

Akizungumza kutoka mkoani Kagera, Maxime amesema ni siku ya 11 sasa tangu kuanza maandalizi katika Uwanja wa Kaitaba ambao ni uwanja wao wanaoutumia katika ligi.

“Mwishoni mwa juma hili tutahama kambi tunakwenda sehemu tulivu kuendelea Uganda tutatafuta michezo ya kirafiki ambayo itanipa mwanga wa kuendelea kuwaona vijana wangu,” amesema Maxime.

Amesema ameongeza wachezaji wachache akiwemo Cleophace Mkandala na Richardson Ng’ondya ili kukipa nguvu zaidi kikosi chake. Aidha Maxime amekiri ligi msimu ujao itakuwa na ushindani zaidi.

“Msimu ujao siyo wa kubweteka upinzani utakuwa mkali sana maana kila timu imejipanga kuhakikisha haishuki daraja na nyingine zinataka kumaliza sehemu nzuri kwenye msimamo,” amesema kocha huyo.

Mwenyekiti wa Simba auawa na wasiojulikana Moro
Jeshi lampindua Rais, lasitisha huduma taasisi zote