Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime amefunguka na kukata mzizi wa fitina baada ya kusema ameamua kutokuuza mchezaji katika timu hiyo na kutoa sababu ni kuhusu mipango yao ya kunyakua kikombe cha ligi kuu Tanzania Bara.

Mexime pia amesema kuwa hata ongeza mchezaji katika kikosi chake akihofia kuwa wageni katika kikosi chake ambapo tayari amekinoa na kimekaa mkao wa kushinda tu.

“Kuongeza wachezaji wapya itanilazimisha kuanza upya kuwapa mafunzo ili waendane na kasi ya wachezaji waliokuwepo katika kikosi”.amesema Mexime.

 

Wanalizombe Wamrejesha Mrwanda Ligi Kuu
Swansea City Wamtimua Garry Monk