Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya (Chadema) amesema kuwa anapendezwa na utendaji kazi wa Rais Dkt. John Magufuli na anaamini kila mmoja anapendezwa na hilo.

Amesema kuwa kuna Watanzania wameaminiwa na wananchi na kupewa kazi ya uwakilishi wanapaswa kumuunga mkono Rais kwa kufanya kazi na si kuacha kazi, kwa sababu wanalitia hasara taifa kwa kurudi kwenye chaguzi ndogo.

Ameyasema wakati akitoa msimamo wake kuhusu tuhuma zinazomkabili kuhusu kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Sasa kama unamuunga mkono Rais fanya kazi kwa bidii, huwezi ukaacha kazi ukae bila kufanya kazi, kazi uliyoaminiwa na wananchi uifanye fanya, sisi Manispaa ya Moshi tunamuunga mkono Rais, na ndio maana napambana kutafuta wawekezaji na tunajenga kiwanda hapa,”amesema Mboya

Hata hivyo, siku za hivi karibuni Meya huyo amekuwa akihusishwa kutimka ndani ya chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.

 

Video: Tundu Lissu huenda akakaa hospitali miezi sita zaidi
Video: Alichozungumza Kakobe, asakwa kwa mahojiano