Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza fedha kiasi cha shilingi Milioni 3.2 zilizotengwa na Halmashauri ya Manispaa hiyo kwa ajili ya kununua bastola ya Mkurugenzi zirejeshwe.

Meya Raibu ametoa tamko hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Stephen Kagaigai ambaye pia alishiriki kikao hicho.

Amesema kuwa fedha hizo zilipitishwa na halmashauri hiyo mwaka 2015 na kubainisha kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Kuna fedha zilipitishwa mwaka 2015 kiasi cha Sh3.2 Milioni kwenye akaunti ya Halmashauri kununua bastola ya Mkurugenzi, haya  ni matumizi mabaya ya fedha za umma, nimeagiza fedha hizi zirudishwe mara moja,” amesema Raibu.

Polisi watupwa jela kwa kumuua mfanyabiashara wa kike
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani chaja na kasi