Meya wa Mji mmoja nchini Bolivia, Patricia Arce, amevamiwa na waandamanaji wa Upinzani na kutembezwa mitaani bila viatu huku akiwa amepakwa rangi nyekundu kisha kukatwa nywele bila hiyari yake.
Tukio hilo limetokea katika vurugu zinazoendelea baina ya Wafuasi wa Serikali na Wapinzani kufuatia kufanyika kwa Uchaguzi wa Rais wenye unaodaiwa kuwa na utata, na hadi sasa watu watatu wanadaiwa kupoteza maisha.
Meya huyo, kutoka chama tawala alikabidhiwa kwa Polisi katika maeneo ya Vinto baada ya kukaa na Waandamanaji hao kwa saa kadhaa na kumfanyia mateso.
Wapinzani walifunga daraja huko Vinto, katika mji mdogo ndani ya Mkoa wa Cochabamba, ikiwa ni sehemu ya kuonesha kupinga uchaguzi uliofanyika Oktoba 20, 2019.
Tetesi zilisambaa kuwa Waandamaji Wapinzani wawili waliuawa kati katika mapambano yaliyotokea karibu na Rais Mteule, Evo Morales , jambo lililozua hasira kwa Wapinzani.
Na walimshutumu Meya Arce kwa kujaribu kuvunja vizingiti vyao walivyokuwa wameviweka dhidi ya wanao unga mkono uongozi wa Rais na pia walimshutumu kuhusiaka na vifo vya wenzao.