Meya wa Jiji la  Dar es salaam, Isaya Mwita ambaye yuko nchini Iran kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Majiji mbalimbali duniani amewakaribisha wafanyabiashara wa Iran kuja kuwekeza nchini.

Mwita ametoa wito huo Jijini Mashahad nchini Iran mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo, amesema kuwa Tanzania ni nchi salama na ina rasilimali nyingi ambazo zitarahisisha uzalishaji kuwa mkubwa.

Amesema kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani na watu wake ni wakarimu ambao hawajawahi kuwa na ubaguzi wowote wa dini, rangi wala kabila na kuwa kila Mtanzania anajivunia umoja huo.

“Watanzania kuna mambo ambayo tulijiwekea tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambapo ndio msingi mkuu ulipoanzia, hakuna ubaguzi wa dini wala rangi, jambo kama hili ni maeneo machache sana katika Nchi zetu kuyakuta, hivyo Tanzania tunajivunia kuwa na utamaduni huu,” Amesema Mwita.

Aidha, ameongeza kuwa Jumuiya za kimataifa zimekuwa zikiwatazama waislam duniani kote kama watu ambao si salama kwa kuwa wamekuwa wakiitumia dini vibaya na ameshauri kuwa haki za binadamu lazima zizingatiwe katika nchi zao.

Hata hivyo katika hatua nyingine Meya amewasisitiza viongozi wa majiji makubwa ya nchi za kiafrika wajielekeze katika kutatua changamoto za watu.

#HapoKale
Salum Mkemi Kufuata Nyayo Za Haji Manara