Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lidume Lihumbo amewataka wafugaji waliopo manispaa hiyo kufuata sheria na taratibu za ufugaji mjini ili kuepuka athari mbalimbali kama vile uchafuzi wa mazingira na ajali ambazo zinaweza kutokea.
Ameyasema hayo mkoani Lindi wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa wafugaji wanatakiwa kufuata sheria zilizowekwa kama vile kutoruhusiwa kuzurura kwa mifugo ya aina yeyote na badala yake wafugaji wanatakiwa kuhifadhi mifugo yao na kuwapelekea chakula katika sehemu ambazo watahifadhi mifugo hiyo.
Amesema kuwa serikali imeweka sheria na adhabu mbalimbali kwa yeyote ambaye atakiuka sheria hiyo kama vile kifungo na adhabu ya faini ili kuleta mabadiliko ndani ya Manispaa ya Lindi.
”Sheria ipo wazi juu ya wale ambao wanaokiuka, mtu akiacha mifugo yake hovyo basi wakamatwe hao na mwenyewe pia atapigwa faini na hata kwa kupelekwa mahakamani kwakuwa sheria ipo wazi na wanaifahamu,” Amesema Lihumbo.
Kwa upande wake mmoja wa wafugaji, Rehema Hatibu mkazi wa Rahaleo mjini humo, amesema kuwa amefurahishwa na sheria iliyopangwa na serikali lakini pia amewaomba wafugaji wenzake kushirikiana kwa pamoja kutii sheria hiyo kwani mifugo inapozurura hupelekea athari mbalimbali katika jamii kama vile uharibifu wa mazao.
-
Serikali yashauriwa kuandaa mpango mkakati wa kunusuru Ziwa Manyara
-
Naibu waziri Mabula agawa vifaa vya kujilinda ngozi Karagwe
-
Nassari ajibu kuhusu kuvuliwa Ubunge
Hata hivyo, Meya wa Manispaa ya Lindi amewasihi wafugaji waichunge vizuri mifugo yao kwani imekuwa ikisababisha ajali barabarani pindi waendapo marishoni.