Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob ametangaza kuwa hatagombea tena nafasi ya udiwani katika uchaguzi ujao.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Meya huyo amewashukuru wananchi kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo, lakini akaweka wazi kuwa hatarejea kwenye kinyang’anyiro.
“Nimetangaza kung’atuka ktk Udiwani kata ya Ubungo Muda wa Madiwani utakapo isha,Sitogombea tena Udiwani Uchaguzi Ujao..! Miaka 10 Utumishi wangu ni Kwa Sababu Wana-Ubungo Mlinikopesha Imani. Tumekuwa wote wakati wa Shida na Raha,Mabonde na Milima #ASANTEUBUNGO #NIMEWASIKIA” ameandika Jacob ambaye ni diwani wa kata ya Ubungo.
Nimetangaza kung’atuka ktk Udiwani kata ya Ubungo Muda wa Madiwani utakapo isha,Sitogombea tena Udiwani Uchaguzi Ujao..!
Miaka 10 Utumishi wangu ni Kwa Sababu Wana-Ubungo Mlinikopesha Imani.
Tumekuwa wote wakati wa Shida na Raha,Mabonde na Milima#ASANTEUBUNGO#NIMEWASIKIA pic.twitter.com/xZ3LuVobbs— Boniface Jacob (@MayorUbungo) April 6, 2020
Hata hivyo, Meya huyo ameeleza kuwa ana mpango wa kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Ubungo, na kwamba anasubiri mchakato kupitia chama chake. Ametoa kauli hiyo alipohojiwa na Mwananchi.