Huyu ni mzaliwa wa Charenton-le-pont nchini UFARANSA. mnamo Oktoba10 1969. Kocha huyu amejizolea umaarufu kwa kiwango kizuri anachokionesha mara kwa mara kwenye vilabu kadhaa anavyopitia.
Mwaka 2013 alitwaa taji la ligi kuu nchini Rwanda akiwa na klabu ya Rayon sports na mwaka 2014 & 2015 Alitwaa taji la ligi ya CAMEROON akiwa na klabu ya Walima pamba ya Cotton Sports Fc.
Baada ya kufanya vizuri nchini Rwanda, maboss wa Rayon sports walilazimika kumuongeza mkataba, jambo ambalo yeye alilikataa kwa kuwa alihisi ameshakamilisha huduma yake nchini humo.
Gomez akajiunga na CS CONSTANTINE ya nchini Algeria kwa kandarasi ya miaka miwili na kuiokoa timu hiyo kushuka daraja kwenye ligi hiyo kwakuwa ilikua na hali mbaya.
Mwezi March 2019 alijiunga na Horoya Ac ya nchini Guinea ambapo hakudumu, alifukuzwa mwezi Novemba kwa sababu za kiufundi na kwa kupoteza mechi 3 kwenye mechi 6 alizocheza na kushinda mbili huku akidroo moja
Tarehe 8 januari 2020 klabu ya ISMAILY SC ikamtangaza Didier Gomez kama kocha wao mpya. Na aliiwezesha timu hiyo kufika Nusu fainali ya kombe la ARAB CUP.
Tarehe 14 December 2020 kocha huyu akajiunga na Al MERRIKH ya Sudan na kuiwezesha kufuzu katika hatua ya makundi. Hali ambayo wasudani waliikosa kwa miaka minne nyuma.
Mafanikio binafsi ya kocha huyu.
Mwaka 2014 Best coach in Cameroon
2015 alikua kocha wa tatu kwa ubora Afrika kwa makocha wa kifaransa.
Kama alivyoondoka Sven Vanderbroek kunako viunga vya msimbazi, ndivyo hivyo alivyon’gamuka kocha huyu kwa waarabu wa Sudan.