Hubert Velud, alizaliwa Juni 8, 1959 katika mji wa Villefranche-sur-Saone, nchini Ufaransa na alianza kucheza soka miaka ya 1970 katika klabu ya Reims. Klabu hii aliichezea kati ya 1976-1989 alipohamia Chalons-sur-Marne iliyokuja kuifundisha pia.

Klabu nyingine alizozifundisha ni Paris FC, gazelec Ajaccio, Clermont, Creteil, Toulon, Beauvais kabla ya kuifundisha timu ya taifa ya Togo kati ya 2009-2010.

Kocha huyo anayesifika kwa soka la kitabuni na lenye kushambulia zaidi, ni mzoefu katika soka la Afrika kwani amezifundisha klabu kadhaa na kutwaa nao mataji kabla ya kutua Sudan anakkoinoa kwa sasa timu ya taifa hilo.

Klabu kubwa alizofundisha Afrika na zinazomfanya kuwa mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa kwa soka la bara hili ni pamoja na Hassania Agadir ya Morocco, ES Setif, US Alger na CS Constantine za Algeria, TP Mazembe ya DR Congo, Difaa El Jajida ya Morocco, aliyowahi kuichezea Saimon Msuva kisha kuhamia JS Kabylie ya Algeria hadi mwaka jana kabla ya kutua Sudan.

Velud ametwaa mataji kadhaa akiwa na timu alizofundisha ikiwamo Clermont ya Ufaransa aliotwaa ubingwa wa Taifa 2001-2002 kisha kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Algeria akiwa na ES Setif mwaka 2013, akabeba Super Cup nchini Algeria akiwa na USM Alger 2013 na ubingwa wa Ligi Kuu 2014 kabla ya kuhamishia makali DR Congo akiwa na Mazembe, likiwamo taji la CAF Super Cup 2016.

Hitimana na mkakati wa kuinusuru Mtibwa Sugar
Kim Poulsen: Safu ya ulinzi imetuangusha