Tarehe 06 mwezi wa 08 mwaka 1989 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alizaliwa mshambuliaji na nahodha wa mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba John Raphael Bocco alizaliwa.
Bocco alilelewa na wazazi wake katika eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Kitaani Gonga FC ndipo kijana mmoja mrefu mwenye sauti ya busara, udongo na nyasi zilibatiza kipaji chake cha ufungaji pia uongozi.
Pande la mtu, urefu futi 6.2, yatosha kuwapa maswali mabeki wanaekutana nae, mTanzania ila mwili kama mtu wa Afrika kaskazini, mitaa ikamuita Adebayor.
Kila kocha aliemfundisha anamuona mchazaji muhimu sana uwanjani, na nje ya uwanja kama kiongozi na mshambuliaji hodari.
Mentality ya uongozi kama Yaya Toure uchezaji na uhodari wa kufunga kama Mario Mandzukic.
Safari ya masiha yake ya soka la ushindani ilianza mwaka 2007 kwa matajiri kiwandani Azam FC, 2008 walifanikiwa kupanda ligi kuu, moja kati ya wachezaji walioipandisha timu akiwemo Sureboy kisha walifanikiwa kuutwaa ubingwa 2014.
Ubingwa huo ni dhahiri kwamba Bocco alikuwa mtu muhimu kama mfungaji na kiongozi, namba 19 mgongoni, standing tall kama Eiffal Tower, a man with incredible Power.
Baada ya miaka 10, mitaa ya msimbazi ikamuhitaji pale Simba SC. Alihamisha magoli na uongozi wake, akavaa kitambaa, wana msimbazi wakamuheshimu, ila nae pia akaiheshimu nembo ya timu katika kifua chake.
Kachukua ubingwa mara mbili mfululizo, mgongoni 22 (11×2) anaongeza kitu special cha pili x ujumla wa wachezaji 11 ndani ya Simba, Hii jezi aliitamka kabla ya kustaafu kocha Joaquin Capparos wa Sevilla na kumsifia.
Mzuri mipira ya juu, anakuwa muhimu pale timu haiwezi kucheza sana mipira ya chini, ndie moyo wa plan B ya Simba.
Unakumbuka cross ya Zana Coulibaly vs Al Ahly akanod header kwa Kagere nae akapiga kibomba wayaa, walete. Bocco alipiga magoti na kushangilia kwa passion.
Kama Mandzukic, anaweza kutokea pembeni, nikukumbushe goli vs As Vita, Niyonzima anampatia Bocco pembeni ya box kama winga, anapiga V-Pass, Niyonzima in-dummy akaisusia kwa Chama nae akaipiga kuta za ndani ya nyavu.
Simba robo fainali, again Bocco kwa Passion katika kibendera alilala akiangalia juu na kushangilia kwa nguvu.
Akistaafu nataman mechi ya kumuaga iwe Azam vs Simba, kipindi cha kwanza acheze Azam cha pili Simba, nitafurahi sana huku nikikupungia mkono wa kwaheri nenda kapumzike“The Captain”