Koboko ndiyo nyoka hatari kuliko nyoka wote hapa duniani na hii ni kwa sababu ya mkusanyiko wa sumu kali alionao, nyoka huyu ana aina mbili za sumu ambazo hufanya kazi kwa pamoja na endapo mtu atang’wata basi ndani ya dakika 3 hadi 10 mtu huyu akikosa matibabu hupoteza maisha.
Nyoka hawa huwa na maeneo maalumu ya kung’ata ambayo ni kichwani, shingoni au kifuani kwani mara nyingi hukaa juu ya mti, na ukiwakuta chini urefu wao ni futi 16 na akiwa na hasira husimama nusu mwili wake ambapo ni sawa na futi 8.
Wataalamu wanashauri jinsi ya kumuua ni kuchemsha chungu cha maji ya moto au uji kisha kujitwika kichwani na kupita maeneo ambao wanapatikana nyoka hawa, wakitaka kung’ata katika maeneo yao huishia kudumbukia ndani ya chungu hiko chenye kimiminika cha moto, hufa.
Lakini pia nyoka huyu unaambiwa anauwezo wa kutembea mwendo kasi mkubwa sana ambapo anaweza kukimbia 23km hadi 25km ndani ya saa moja, huku binadamu wa kawaida ana uwezo wa kukimbia 12km ndani ya saa moja na endapo mnyama huyu ataamua kung’ata sehemu yenye kundi kubwa la watu basi anauwezo wa kung’ata kunzia watu/wanyama 70 nakuendelea bila kuchoka.
Hapa nchini kwetu nyoka aina hii hupatikana kwa wingi mkoani Tabora na sehemu zenye misitu mikubwa kama vile, Iringa, Morogoro, Milima ya Udzungwa huko wapo wegi sana.
Pia nyoka aina hii hutajwa katika orodha ya wanyama wanaoongoza kuuwa watu wengi zaidi duniani.
Na unaambiwa nyoka huyu akiwa msituni hapendelei kusikia kelele au milio ya gari na mara nyingi endapo atasikia mlio wa gari hupendelea kuufuatilia mlio huo nakufanya shambulio hivyo inashauriwa kufunga vizuri vioo vya magari wakati wa kupita msituni.
Na wataalamu wanashauri kuwa endapo nyoka huyu atakuwa amejificha katika upenyo wa gari basi ni vyema dereva kukimbiza gari hilo kwa mwendo kasi usiopungua 80 na kuendelea kwa ndani ya dakika 10 hadi 15 ili kusaidia kummaliza nyoka huyo kutokana na joto kali au kumchosha nyoka huyo na kumpunguzia makali ya sumu yake ya kudhuru watu.