King Mswati wa iii wa Swaziland amekanusha juu ya tamko lake lililosambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamiii la kuwataka wanaume nchini kwake wenye umri wa kuoa, waoe wanawake wawili au zaidi kuanzia juni mwaka huu na kusema atakayeenda kinyume na agizo hilo kufungwa jela.
Kwa mujibu wa msemaji wa Serikali ya mfalme Mswati, Percy Simelane amesema kuwa Serikali nchini humo haijawahi kuzungumza suala hilo.
Hata hivyo stori iliyotolewa siku ya jumatatu ilisema Serikali itatoa msaada kwa wanaume waliooa wanawake zaidi ya mmoja kwa kuwapa nyumba na kugharamia harusi zao.
Aidha tamko hilo liliweza kuaminiwa na watu wengi kutokana na historia ya mfalme Mswati ya kuwa na wake 15 na watoto 25, huku Baba yake ambaye alimuachia urithi wa kiti hiko cha ufalme alikuwa na wake 70 na watoto 150.
Hata hivyo nchi hiyo inatajwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake na idadi ndogo ya wanaume na kupelekea wanaume angalau kuoa wake wawili au zaidi.