Nahodha wa Kambi ‘GYM’ maarufu ya ndondi ya Nakos Bondia Mfaume Mfaume ameondolewa kwenye orodha ya ubora wa mabondia (Kitaifa na Kimataifa) kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa duniani (Boxrec).

Boxrec imemtaja Mfaume kuwa bondia ambaye hachezi mara kwa mara ndondi, huku ikimuondoa kwenye nafasi ya kwanza nchini katika uzani wake wa Middle na kumfuta kwenye viwango vya kimataifa.

Hata Hivyo Mfaume Mfaume amekiria kupokea taarifa za kuondolewa kwenye ‘Boxrec’ lakini amesisitiza atarudi kutokana na mipango iliopo hivi sasa ya kutaka kupanda ulingoni.

Amesema anaamini changamoto za kutokupanda ulingoni kwa muda mrefu ndizo zimesababisha kuondolewa kwenye orodha hiyo ya viwango vya ubora, hivyo amewataka mashabiki wake kumuamini na kuendelea kumpa ushirikiano.

“Naamini Nitarudi, na nitakuwa bora zaidi” amesema Bondia Mfaume Mfaume

Mara ya mwisho Bondia huyo alipanda ulingoni April 08 mwaka 2021 na kupoteza dhidi ya Rizvan Nical kwa Knock Out (TKO) ya raundi ya pili.

Mbali na Mfaume, baadhi ya mabondia maarufu nchini walioondolewa kwenye viwango ni pamoja na Mada Maugo anayepigania uzani wa cruiser na Japhet Kaseba aliyewahi kuwa namba moja kwenye uzani wa Light Heavy.

Kim Poulsen: Tanzania ina nafasi AFCON 2023
Barbara Gonzalez atangulia Afrika Kusini