Uongozi wa klabu ya Young Africans umefungua milango kwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti na Mdhamini wa klabu hiyo, Yusuph Manji ili kuongeza nguvu katika mchakato wa uwekezaji.

Young Africans imetoa kauli hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu CPA Haji Mfikirwa ambapo amesema, Manji ana uhuru wa kurudi klabuni hapo kwa sababu hakufukuzwa kwa misingi ya kikatiba.

“Kama Manji atakuja hatofukuzwa na hakuwahi kufukuzwa Young Africans wala hakuna msimamo wa sekretarieti au uongoz i wa juu, kuwa Manji akihitaji kurudi hatapewa fursa, hivyo milango ipo wazi kwake kurudi” amesema Mfikirwa na kuongeza:

“Cha muhimu tu ni kukidhi vigezo, na mfumo wetu wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu unaruhusu wawekezaji zaidi ya mmoja, hivyo akitaka kurudi klabu haina neno, aje na sisi yetu, yeyote mwenye sifa za kuwekeza Young Africans anaruhusiwa.” Amesema CPA Mfikirwa.

Taarifa zinaeleza kuwa Manji yupo Bongo na hesabu zake kubwa pia ni kurejea katika uwekezaji ndani ya kikosi cha Young Africans.

Juni 27, Wanachama wa Young Africans wanakwenda kwenye mkutano wa mkuu, huku moja ya ajenda ikiwa ni mabadiliko na inatajwa kuwa huenda tajiri huyo akaibukia ndani ya mkutano huo.

Bumbuli: Nilikua natania
Mawaziri wa Fedha nchi za G7 kukutana London