Mara baada ya mvua kubwa kulisomba daraja la kiyegeya  barabara ya Morogoro-Dodoma Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchi (TANROADS), Patrick Mfugale amesema barabara hiyo ni chakavu.

Ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kumuondoa katika nafasi yake Meneja wa TANROADS-Morogoro kwa madai ya kutokagua miundombinu na hivyo daraja hilo lililopo Kilosa kusombwa na maji.

Mfugale, ambaye ni mtaalamu wa Ujenzi amesema barabara hiyo ilijengwa miaka 40 iliyopita na hivyo imeshatumika muda mrefu ndio maana kila mara wamekuwa wakiifanyia ukarabati.

Amesema kuwa kukatika kwa daraja hilo ni kutokanan na uchakavu wa daraja na kwamba ni jambo la kawaida ambapo amesema kuwa kitaalamu uhai wa makalavati yanayowekwa si zaidi ya miaka 25 na kuwa tayari Serikali iko katika mchakato wa kuijenga upya barabara hiyo na madaraja yake.

Chadema kuvaa nguo nyeupe
Uhakiki wa vyama vya siasa kuanza rasmi