Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake inakusudia kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa umma kupunguza utegemezi wa mashirika ya umma kwa Serikali.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Agosti 19, 2023 wakati akifungua Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kinachofanyika katika Ukumbi wa AICC – Arusha.

Amesema, “Serikali imepanga kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa umma kama njia ya kupunguza utegemezi [wa mashirika ya umma kwa serikali] tukiamini mpango huu utakuwa na faida kubwa kwa nchi yetu.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 20, 2023
Polisi wawafariji Wagonjwa Hospitali kuu ya Jeshi