Shirika la Umeme (TANESCO) limesema kuanzia Julai mwaka huu litakuwa na mfumo wa ununuzi wa umeme ambao utawezesha wateja wao kuweka umeme kwenye mita papo hapo (automatically) tofauti na wa sasa unaohitajika ‘token’ kuingizwa kwenye mita zao.
Mkurugenzi wa TEHAMA wa shirika hilo, Cliff Maregeli, amesema kuwa mfumo huo unaotarajiwa kuanza na majaribio kwa kubadili mita na kuweka mpya zenye uwezo wa kusoma mfumo wa TANESCO.
Maregeli amesema kwamba mita zilizopo sasa hazina mfumo wa kisasa kubaini masuala mbalimbali ikiwamo eneo ambako umeme umekatika au mteja amekosa huduma kutokana na kuchelewa kulipia huduma.
“Mita tulizonazo sasa hivi hazina uwezo wa kuongea na mifumo ya TANESCO. Sasa ukinunua umeme utahitajika kutafuta njia ya kuufikisha umeme nyumbani kwako. Tunakuja na njia ambayo tumeweka, tukikupa wewe inajua hiyo tokeni ni ya kwetu.