Serikali imepunguza faini ya kupitiliza muda wa malipo ya maegesho kutoka Sh30,000 hadi Sh10,000 huku muda wa malipo ukiongezwa kutoka Siku 7 hadi 14 ambapo mfumo wa malipo ya maegesho unatarajiwa kuanza Desemba mosi mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu, Novemba 5, 2021wakati akiongea na waandishi wa habari.
Waziri Ummy ameagiza uhakiki wa madeni katika magari kabla ya mfumo huo kusitishwa.
Amesema kuwa baada ya uhakiki wa madeni hayo mapendekezo yapelekwe Wizara ya Fedha.
“Madeni yanafikia Sh811 milioni, tunaangalia utaratibu wa kufuta madeni yaliyojitokeza kutokana na changamoto za mfumo huo, tunafanya uhakiki kisha yatafutwa kwa mujibu wa taratibu za Serikali” amesema Waziri Ummy.