Mabingwa wa soka Ligi Kuu ya wanawake Tanzania Bara, Simba Queens wameanza kujizatiti kwa msimu ujao kwa kumsajili mlinda mlango wa kutumainiwa wa timu ya taifa ya wanawake ya Uganda, Ruth Ataro.

Mratibu wa timu hiyo, Selemani Erasssy, amesema tayari wamefanya mazungumzo na kipa huyo ambaye amekubali ofa ya Simba, na wakati wowoteatasqaini mkataba wa kujiunga na Simba Queens.

Amesema baada ya kutuma ofa yao kwa kipa huyo, ameridhia na anatarajiwa kuwasili nchini na kusaini mkataba wa kukitumikia kikosi cha timu yao hiyo kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake.

“Kila kitu kuhusu mchezaji huyo kinaenda vizuri tunatarajia wiki hii atakuja nchini kwa ajili ya kusaini pamoja na kuwa miongoni mwa wachezaji watakaotambulishwa katika Sherehe za ‘Simba Day,” amesema Erassy.

Amesema pia wako katika mchakato wa kusajili wachezaji wawili wa ndani ambao hakutaka kuwaweka wazi kwa madai kuwa kuna baadhi ya timu wanahitaji huduma za nyota hao.

“Hatufanyi usajili mkubwa ukizingatia kwa wachezaji wa ndani viwango vinalingana, pia kwetu tulikuwa tunahitaji kipa mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya kimataifa hali ambayo tumerudi kwa mara nyingine kwa Aturo ambaye msimu uliopita ilishindikana kumpata kwa sababu alikuwa anasoma chuo,” amesema Erassy.

Young Africans Vs Simba SC - OKTOBA 18
Lebanon: Rais Aoun akata kujiuzulu