Mganga wa kienyeji mkoani hapo, Juma Kipanya anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi na kukatisha ndoto ya kuendelea na masomo.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapo, Foka Dinya, amesema kuwa wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo ili afikishwe mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili, likiwamo la kumkatisha masomo mwanafunzi huyo.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 alikuwa anaingia darasa la saba na inadaiwa kupewa ujauzito na mganga huyo mwishoni mwa mwaka 2021, baada ya kuitwa na mganga huyo kusaidia kutengeneza dawa za kutibu ugonjwa uliokuwa unamsumbua babu yake.
Kaimu Kamanda Dinya akizungumzia taarifa za mganga huyo, alisema wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu mashtaka yanayomkabili, likiwamo la kubaka, kumpa ujauzito na kukatisha ndoto za mwanafunzi huyo.