Kampuni ya Madini ya dhahabu ya Geita Gold Mine (GGM) imejipanga kutumia Shil 9.2 bilioni mwaka wa fedha 2019/20 kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wanaoishi karibu na mgodi huo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Richard Jordinson katika hafla ya kutiliana saini ya makubaliano na halmashauri mbili za wilaya ya Geita.

Amesema kuwa fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi ya afya, mazingira, elimu, kilimo na miundombinu.

Aidha, amesema kuwa mgodi huo unaamini kufanyakazi kwa pamoja na jamii inayowazunguka ili kuwa na uwajibikaji wa pamoja katika kutekeleza na kuitunza miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema kuwa GGM ni kampuni ya kwanza iliyotii agizo la serikali linalozielekeza kampuni za madini kuandaa mpango unaoaminika wa uwajibikaji wa jamii (CSR)

Hata hivyo, Gabriel ameongeza kuwa mapato yatokanayo na mgodi yamesaidia halmashauri ya mji kuongoza kwa mapato kwa kukusanya asilimia 157 na kuifanya kuwa miongoni mwa halmashauri tano zilizopeleka mapato yake kwenye miradi ya maendeleo kwa wananchi.

 

Tanzania yapongezwa kwa kukidhi vigezo vya uchumi vya SADC
Habari Picha: Matukio mbalimbali yanayoendelea katika mkutano mkuu wa SADC