Waziri Mkuu wa zamani wa Sudani Abdalla Hamdok, amesema mapigano katika nchi yake yatakuwa jinamizi kwa ulimwengu iwapo yataendelea na kuonya kuwa mzozo unaweza kuwa mabaya zaidi kuliko wa Syria na Libya.

Akizungumza katika mkutano katikka mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Hamdok alitoa wito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja za kimataifa ili kumshawishi kiongozi wa kijeshi wa Sudan na mkuu wa kikosi pinzani cha kijeshi kufanya mazungumzo ya amani.

Abdalla Hamdok alihudumu mara mbili kama Waziri Mkuu wa Sudan kati ya 2019 na 2022

“Hii ni nchi kubwa, tofauti sana … nadhani itakuwa jinamizi kwa ulimwengu,” alisema.

“Hivi sio vita kati vya jeshi na uasi mdogo. Ni karibu kama majeshi mawili yenye mafunzo ya kutosha na yenye silaha.”

Hamdok ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu mara mbili kati ya 2019 na 2022 – aliongeza kuwa ukosefu wa usalama unaweza kuwa mbaya zaidi kuliko vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria na Libya.

Mapigano hayo ambayo yamedumi kwa takribani wiki mbili yamesababisha vifo vya mamia, huku makumi ya maelfu ya watu wakiikimbia nchi yao.

Alhamisi usiku wa muda wa usitishaji vita kati ya pande zinazohasimiana ulifuatia juhudi kubwa za kidiplomasia za nchi jirani, pamoja na Marekani, Uingereza na Umoja wa Mataifa.

Lakini nyongeza ya saa 72 haijafanyika.Mashambulio ya anga, vifaru na mizinga yanaripotiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo ya Khartoum.

Jeshi la Sudan linasema kuwa linashambulia mji mkuu Khartoum kutoka pande zote, kwa kutumia silaha nzito nzito.

AS Roma yamuweka sokoni Paul Dybala
Mkuu wa shule apiga ramli shuleni