Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Roots nchini Kenya, Profesa George Wajackoyah ameendelea kujitangaza na kunadi kampeni zake kwa kutangaza misimamo mikali itakayochukuliwa na serikali yake akishinda uchaguzi wa Agosti.
Wajackoyah mwenye umri wa miaka 61 na mgombea mwenza wake Justina Wangui Wamae ni mmoja wa wagombea wanne wa urais walioidhinishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka yan Kenya (IEBC).
Katika ahadi zake kwa wakenya, Wajackoyah anataja kuhalalisha bangi ili kuimarisha kipato cha taifa na kulipa deni la Kenya inalodaiwa inalodaiwa na uchina.
Wajackoyah alihoji kuwa iwapo Wakenya wataruhusiwa kukuza bangi kwa lengo la kuuza katika soko la kimataifa, taifa la Kenya ilitakuwa na pesa kwani gunia moja la zao hilo linauzwa wa dola milioni 3.2.
“Suluhisho la deni kubwa la taifa ni ukuzaji wa bangi ambayo itasaidia nchi hii kulipa deni lote,”
Pia mgombea huyo ameahidi ufugaji wa nyoka akisema itaimaarisha kipato cha taifa kwa kuwa sumu itatolewa kwa wanyama hao na kutumiwa kutengeneza dawa huku nyama yake ikiuzwa katika mataifa ya nje kama vile Uchina.
“Tuna walaji wengi wa nyoka kama vile Wachina. Njia moja ambayo tutatumia kumaliza deni la uchina ni kutoa sumu kutoka kwa nyoka hao na kuwapa Wachina nyama waile na kuwaambia wajilipe,” Wajackoyah alisema.
Msomi huyo anatarajia kuminyana na Naibu Rais William Ruto (UDA), Raila Odinga (Azimio) and David Mwaure Waihiga (Agano).