Mgombea Urais wa JMT kupitia tiketi ya Chama cha NCCR- Mageuzi Jeremiah Maganja ameahidi kubadilisha Sheria kandamizi endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania ifikapo Oktoba 28, 2020.

Maganja amesema akipata ridhaa, ataboresha Uchumi wa Taifa na kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara huku akifuta Vitambulisho vya Bima ya Afya na kwamba amegundua wengi walionavyo hawanufaiki na matibabu.

Hata hivyo Maganja ameahidi kufuta michango na wanafunzi watasoma bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo.

Ameongeza kuwa, atahakikisha walimu wanaenda semina za mara kwa mara ili kuwasaidia kukabiliana na mitaala ya Kisayansi.

Cristiano Ronaldo afanyiwa uchunguzi Italia
Mourinho aipinga VAR hadharani

Comments

comments