Mgombea urais wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, pamoja na timu yake ya kampeni, wamekamatwa na polisi eneo la Kalangala katikati ya nchi hiyo.

Kukamatwa kwa Bobi Wine ambaye ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter kumezusha maandamano katika kisiwa cha Kalangala ambako helikopta ilitua na wafuasi wa Bobi Wine wamesema wanaamini ingetumiwa kumsafirisha hadi Kampala.

Maafisa wa polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji.

Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo lakini ambaye hakutaka kutambulishwa, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba maafisa wa polisi walifyatua pia risasi kuwatawanya waandamanaji barabarani.

Bobi Wine ameibuka kuwa mshindani mkali wa Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, kuelekea uchaguzi mkuu wa Januari 14.

Serikali yasitisha makongamano, mikutano ya mkesha wa mwaka mpya
ATCL kuanza safari Chato-Dar