Mgombea wa udiwani wa Chadema Kata ya Sofia wilayani Malinyi, Riko Venance amewekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi baada ya kutembelea kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi Mission.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alfonce Mbassa, ambapo amesema kuwa mpaka sasa hajaambiwa mgombea huyo anashikiliwa na polisi kwa kosa lipi.

“Nimepewa taarifa kuwa mgombea wetu anashikiliwa na jeshi la polisi, sasa hivi ndio naelekea huko sijajua tatizo ni nini, nitatoa taarifa baadae,”amesema Mbassa

Aidha, Kata ya Sofia ina vijiji vitatu ambapo viwili vinaongozwa na Chadema wakati kimoja kilishindwa kufanya uchaguzi kwa sababu ya migogoro.

JPM amuandikia barua Rais wa China
Video: Rais Dkt. Magufuli amwambia Pinda ukweli mchungu, CCM, Chadema nani mbabe?