Vyama vya wafanyakazi Ufaransa vimeanza mgomo wa nchi nzima kuanzia leo Jumanne Oktoba 18, 2022 kudai nyongeza ya mishahara kufuatia hali ngumu ya maisha inayotokana na mfumuko wa bei.
Mgomo huo, unamuweka rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron katika changamoto kubwa kwa mara ya kwanza, tangu alipochaguliwa tena kuiongoza Ufaransa mapema mwezi Mei, mwaka huu (2022).
Mgomo huo kimsingi utaathiri shughuli katika sekta ya umma kama shule na usafiri. Ni hatua ya mwendelezo wa wiki kadhaa zilizochukuliwa na sekta ya kiviwanda ambazo zimevuruga shughuli katika viwanda vikubwa vya kusafisha mafuta vya nchi hiyo.
Inaarifiwa kuwa, hali hiyo imesababisha vituo vingi vya uuzaji mafuta ya Petrol kukabiliwa na hali ngumu ya usambazaji wa nishati hiyo na kwamba raia wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za huduma za juu za bidhaa.