Mhasibu wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph, Elizabeth Asenga jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na tuhuma za kumkashfu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa Whatsap.

Wakili wa Serikali, Leonard Challo aliiambia mahakama hiyo kuwa Mtuhumiwa alifanya kosa hilo kwa kuandika ujumbe wenye kashfa kwa Rais Magufuli huku akijua ni kosa, katika kundi (group) la Whatsap la STJ Staff Social Group.

Wakili Challo aliusoma ujumbe huo uliodaiwa kuandikwa na Elizabeth Agosti 6 kuwa, “Good morning humu. Hakuna Rais kilaza duniani kama huyu wetu duniani. Angalia alivyompa Lissu umashuhuri, f** lile, picha yake ukiiweka ofisini ni nuksi tupu. Ukiamka asubuhi, ukikutana na picha yake ya kwanza siku yako inakuwa mkosi mwanzo mwisho.”

Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kwua na wadhanamini wawili wenye dhamana ya shilingi milioni 2 kila mmoja.

Wakili Challo aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, na kesi iliahirishwa hadi Septemba 22 mwaka huu.

 

Video: Waziri Mkuu atembelea kituo cha tiba cha kimataifa (MUHAS)
NHC kupiga mnada mali za Mbowe