Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt.  Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kuandaa mpango mkakati wa  kurekebisha makambi ya JTK, na kuanza ujenzi haraka.

Rais Samia qmetoa maagizo hayo hii leo Julai 10, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya ya Miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa – JKT, kilichofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT.

Amesema, “Jkt siku zote imesimama imara katika kulipigania Taifa letu katika kuboresha Amani na mshikamano kuanzia Dini, kabila na Jinsia hivyo na Serikali haitaacha kuwaunga mkono katika mambo mbalimbali ambayo mnafanya.”

Rais Samia ameongeza kuwa, JKT inakwenda kutekeleza mpango wa tatu wa miaka mitano wa maendeleo  ambao utamalizika 2027 leongo kubwa ikiwa ni kuchagiza wajibu wa kila Mtanzania kutumia rasilimali za ndani ili kujitosheleza na matakwa yetu ili kuondoa utegemezi. 

Gwaride la Jeshi la Kujenga Taifa likipita mwendo mbele ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan wakati wa Maadhimisho ya kilele cha Miaka 60, ya JKT Jijini Dodoma.

“Tuna Jeshi lenye uwezo mkubwa  na lenye ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha mpango huo wa miaka mitano tunafanya mambo makubwa,Na tumeona Baadhi ya kazi zilizofanywa na jeshi la jkt tWameweza kujenga ukuta wa mireraani, tumeona ujenzi wa Ikulu katika Mji wa Mtumba,” Ameongeza Rais.

Awali, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amesema Wizara itaendelea kuboresha elimu ilikuwa na bunifu mbalimbali na kuwa na vijana wengi wenye bunifu.

Amesema, “ Wizara pia itaendelea kuendeleza michezo ilikuendelea kuibua vipaji mablimbali katika jeshi la kujenga Taifa na vilevile tumejizatiti katika uzalishaji chakula  ili kujitegemea wenyewe katika suala la uchuni na chakula.”

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi  laya Ulinzi  na Usalama, Jenerali  Jackob Mkunda amesema kwa Mwaka huu (2023), namba ya Vijana walioingia kwa mujibu wa sheria imeongezeka kwa asilimia kubwa ikiwa ni mafanikio makubwa ndani ya kipindi cha miaka 60 ya JKT.”

“Hivyo tunaendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutenga bajeti kwa kila mwaka ya kuendelea kurekebisha miundo mbinu ambayo leo hii imefanya tumepokea vijana wengi,” amesema Jenerali Mkunda.

Kijana afa maji akijaribu kuogelea
Uwekezaji, ulinzi wazikutanisha Tanzania, India