Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) imessema kuwa imenufaika na mabadiliko chanya yaliyofanyika ndani ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mabadiliko hayo yameboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa na mazingira bora kwa watoa huduma jambo ambalo limeleta faraja kwa wananchi wanaofika kwenye taasisi hiyo kupata huduma mbalimbali za tiba ya mifupa.

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa MOI, Jumaa Almasi  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo kwenye miaka miwili ya uongozi wa Rais Magufuli.

“Maboresho yaliyofanyika katika kipindi hiki kifupi yameiwezesha MOI kutoa huduma bora kwa wakati ukilinganisha na miaka mingine iliyopita,” amesema Almasi.

Aidha, amesema kuwa idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji imeongezeka hadi kufikia wagonjwa 700 kwa mwezi kutokana na Serikali kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba na nafasi ya kulaza wagonjwa.

Kwa upande Afisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi ameseka kuwa pamoja na upasuaji mkubwa uliofanyika katika kipindi hiki pia viungo bandia 1,362 vimetengenezwa kutokana na Serikali kurahisisha upatikanaji wa malighafi za kutengenezea viungo hivyo.

.

Moyes alamba shavu West Ham
Dkt. Kigwangalla aapa kuwashughulikia wala rushwa