Kiungo Michael Carrick anapewa nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi cha Man Utd ambacho mwishoni mwa juma hili kitacheza mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England, dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.

Meneja wa Man Utd, Louis van Gaal amethibitisha kuwa katika harakati za kumtumia kiungo huyo, kutokana na hali yake kuendelea vyema baada ya kujiuguza maumivu ya misuli ya mwili kwa siku kadhaa zilizopita.

Van Gaal, amesema anajihisi mwenye furaha kuwa na matarajio ya kumtumia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 katika mchezo huo, na anaamini uzoefu alionao utakisaidia kikosi chake kupambana vyema na kuondoka na point ugenini.

Carrick, alikua nje ya kikosi kilichocheza mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya siku ya jumatano dhidi ya Wolfsburg ambao walikubali kufungwa mabao mawili kwa moja kwenye uwanja wa Old Trafford.

Tz Bara Kushiriki Challenge CUP Mwezi Novemba
Utaupenda Ujumbe Wa Zari Kwa Diamond Kwa Ajili Ya ‘Birthday’ Yake Leo