Kiungo kutoka nchini England, Michael Carrick amesaini Mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea Manchester United chini ya kocha mpya, Mreno Jose Mourinho.

Man United imethibitisha kiungo huyo iliyemsajili kutoka Tottenham mwaka 2006, amekubali kuongeza mkataba utakaomuweka Old Trafford hadi Juni 2017 kukamilisha miaka 11 ya kuwatumikia Mashetani Wekundu.

Katika kipindi chake cha miaka 10 Man United hadi sasa, mchezaji huyo ameshinda mataji matano ya Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Ligi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.

“Hii ni klabu kubwa na imekuwa sehemu ya maisha yangu kwa miaka 10 iliyopita, hivyo nina furaha safari hii nzuri inaendelea,” amesema Carrick.

Pia akaelezea furaha yake ya kuingia katika zama mpya za kufanya kazi na kocha mpya, Jose Mourinho ambaye aliteuliwa mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Mholanzi, Louis van Gaal.

Video: ‘zigo remix’ ya Ay na Diamond imefanywa upya Kenya, Hii hapa Video yake
Young Africans Yatuma CAF Majina Ya Wachezaji Wanne