Mke wa Rais mtaafu wa Marekani Barack Obama, Michelle amemshambulia kwa maneno Rais Donald Trump, wakati chama cha Democrats kikiwa kimeanza rasmi kampeni ambapo Joe Biden ndiye aliyepewa jukumu la kuwa mgombea wa chama hicho kuelekea Ikulu.

Michelle ambaye hotuba yake ilikuwa imerekodiwa kabla ya Biden kutangazwa mgombea mwenza, Seneta Kamala Harris, siku sita zilizopita, alianza kwa kumshambulia Rais Trump kwa maneno.

“Donald Trump sio rais sahihi kwa nchi yetu, Huwezi kudanganya mienendo yako Uchumi wetu unadidimia kwasababu ya virusi ambayo huyu rais alivipuuza kwa muda mrefu” amesema Michell

“Kusema ukweli ulio wazi kwamba maisha ya mtu mweusi ni muhimu bado ni jambo linalofanyiwa dhihaka katika ofisi ya juu, tunapogeukia Ikulu kwa uongozi, au kutaka kupata faraja, au kupata nguvu ya uimara, badala yake tunachopata ni ghasia, mgawanyiko na ukosefu wa uelewa kabisa.”

“Donald Trump rais stahiki kwa nchi yetu amekuwa na wakati mwingi sana kujidhihirisha kwamba anaweza kufanya kazi hii, lakini ni wazi kwamba mambo yamemzidi unga, hawezi kuwa yule mtu ambaye sisi tunamtaka awe kwa ajili yetu.”Hivyo ndivyo ilivyo.” amesema Michell

Hata hivyo Michell Obama aliitumia fursa hiyo kumpigia debe mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, akimwelezea kama mtu mwenye sifa za kumaliza misukosuko ambayo amesema imesababishwa na utawala wa Rais Trump.

Vyombo vya habari hamasisheni wananchi- NEC
Miaka mitano ya kujivunia sekta ya elimu