Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, imeubuka mshindi wa sita kitaifa pamoja na kupatiwa kombe na Medali kwenye mashindano ya kitaifa ya shirikisho la michezo Serikali za mitaa Tanzania Shimisemita ambayo yamefanyika Jijini Dodoma.

Akisoma taarifa ya wakati wa mapokezi ya timu ya Muleba katika ukumbi wa Halamshauri ya Wilaya hiyo Nahodha Mosses Kuyella amesema wamekuwa na jumla ya michezo tisa na zote wameweza kuingia nane bora na nyingie kufikia hatua ya nusu fainali.

Hata hivyo, ameendelea kusema kuwa wameweza kupata kikombe cha mshindi wa tatu kwa kuvuta kamba kitaifa na kupata medali ya mshindi wa tatu wa riadha ambapo kwa kipindi cha miaka kumi timu hiyo ya Muleba ilikuwa haijawahi kushiriki mashindano hayo ya kitaifa kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Justus Magongo ameagiza ofisi ya utamaduni na sanaa kuendelea na zoezi la kutafuta wachezaji wengine ili kuwaunganisha kuwa nguvu moja.

CCM wakerwa usuaji wa miradi, wizi wa vifaa
Zanzibar yajipanga fursa Utalii wa Mikutano