Michuano ya Safari Lager Cup inaendelea ambapo sasa ipo katika ngwe ya pili kutafuta wachezaji 16 kati ya 22, waliochanguliwa kucheza katika mikoa minne ya Mbeya, Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.

Katika kuendeleza vipaji vya vijana kusaka Mabingwa Wapya Katika Soka ndani ya Safari Cup, Vijana 22 wenye vipaji watachaguliwa kutoka mikoa hiyo, ili kujenga ‘cream dream team’ ya Safari Champions, itakayocheza na timu kubwa ya kimataifa hapo baadae.

Makocha pamoja na Watumiaji wa bia ya Safari Lager na wapenzi wa soka kiujumla, watawapigia kura vijana hao, ili kuchagua viijana hao 22 mabingwa wapya wa Soka.

Aidha, Jumamosi ya Januari 20, 2024 muendelezo wa michuano itafanyika ndani ya Arusha katika viwanja vya Ngarenaro kuanzia saa 10 jioni na Dar es Salaam katika viwanja vya Kinesi kuanzia saa 10 jioni.

Geita Gold yakimbilia Morogoro
Mastaa Kagera Sugar mtegoni