Mshiriki kutoka nchini Ujerumani, Dustin Brown, ameushangaza ulimwengu baada ya kumtoa nishai gwiji wa mchezo wa tennis kutoka nchini Hispania, Rafael Nadal katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa michuano ya Wimbledon inayoendelea jijini London nchini Uingereza.

Brown, ambaye ni mzawa wa nchini Ujerumani alikuwa hapewi nafasi ya kumchakaza gwiji huyo, lakini alifanikiwa kuibuka kinara kwa ushindi wa seti tatu kwa moja ambazo ni 7-5, 3-6, 6-4 na 6-4.

Hata hivyo mchezo huo ulitarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kumbukumbu kuonyesha kwamba Nadal aliwahi kumshinda Brown katika hatua ya mzunguko wa pili mwaka 2014, hivyo kulikuwa na haja kwa mshiriki huyo kutoka nchini Ujerumani kulipiza kisasi.

Wadadisi wa mchezo wa tennis duniani wamekizungumzia kitendo cha Nadal kuondoshwa mapema katika michuano ya Wimbledon, anguko la wakongwe na inaonekana wanaochipukia wapo mbioni kuchukua nafasi.

Nadal, ameshindwa katika mchezo huo ikiwa nia baada ya miaka 10 kupita ambapo imeshuhudiwa akifungwa na mpinzani ambaye yupo zaidi ya nafasi ya 100 katika viwango vya ubora duniani.

Brown, kwa sasa anashika nafasi ya 102 duniani na kitendo cha kumbanjua Nadal kitampandisha na kuingia kwenye 100 bora.

AC Milan Wakamilisha Usajili Wa Mfumania Nyavu Kutoka Brazil
Bilic Aanza Kazi Kwa Mbwembwe Upton Park