Kero wanazopata wafanyakazi kwa kucheleweshewa malipo ya mafao yao na mifuko ya jamii baada ya kuacha kazi au kustaafu imepelekea Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii (SSRA) kuichorea mstari mifuko hiyo ya jamii ili kumaliza kero hiyo.

SSRA imeipa siku 21 mifuko hiyo ya Jamii kuhakikisha inalipa wanachama wake wote ambao malipo ya mafao yao yalicheleweshwa.

Mkurugenzi wa SSRA, Irene Isaka amesema kuwa pamoja na kulipa mafao kwa wanachama waliocheleweshewa mifuko hiyo pia inatakiwa kufuata sheria iliyounda Mamlaka hiyo na kuwalipa kwa wakati wanachama wote waliokidhi vigezo.

Mifuko iliyotajwa kuhusika na ‘dedilaini’ hiyo, ni PPF, PSPF, EGPF, NSSF, LPAF, FEPF NHIF na WCF.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameendelea kushirikilia msimamo wake kuwa mifuko yote ya jamii ingeunganishwa na kuwe na mifuko miwili tu.  Mmoja uwe kwa ajili ya sekta ya Umma na mwingine sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Hotuba ya Rais Magufuli yazua 'Zogo', Wadai kaiteka mahakama kwa ahadi ya fedha
Kikwete kuiachia CCM mapema