Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesisitiza mifumo ya matibabu kuanzia ngazi ya vituo vya afya hadi ngazi ya Hospitali za Taifa isomane, ili kupumguza matumizi mabaya ya fedha za Mifuko ya Bima ya Afya nchi.
Dkt. Mollel ametoa wito huo, jijini Dodoma katika kilele cha kutimiza miaka 12 ya utekelezaji wa mradi wa HPSS- Tuimarishe Afya unaotekelezwa nchini kwa ufadhili wa serikali ya Uswis.
Amesema, “tunahitaji kufika mahali mifumo ya afya isomane katika ngazi zote itasaidia kupuguza matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa bima ya afya kwasaabu hakutakuwa na haja ya kurudia vipimo pasipo kuwa na sababu ya msingi.”
Hata hivyo, amesema kwasasa nchi inaelekea kwenye mfumo wa Bima ya Afya kwa wote, hivyo watakuwa makini kutokutumia fedha kwenye mambo ambayo sio ya msingi, ndio maana wananasisitiza mifumo isomae, ili bima ya afya kwa wote kufanya kazi kwa ufanisi.