Miili 10 zaidi imefukuliwa katika msitu wa Shakahola ikiwa ni siku ya pili baada ya kuanza kwa awamu ya nne ya ufukuaji wa makaburi ya halaiki huko Shakahola nchini Kenya.
Idadi hiyo inafanya miili iliyofukuliwa kwa siku mbili mfululizo kufikiwa maiti 22 hivyo kuwa na jumla ya miili 372 ambapo 338 kati ya hiyo ikiwa tayari ishafanyiwa uchunguzi wa kisayansi kubaini kiini cha kifo.
Miili 12 ilifukuliwa Julai 10, 2023 katika msitu wa Shakahola katika awamu hiyo ya nne ya ufukuzi ulioanzishwa Jumatatu, ikiwa ni wiki mbili baada ya maafisa wa upelelezi kumaliza upasuaji wa maiti 338.
Mauaji haya ya halaiki sio ya kwanza kufanyika kwani historia inaonesha mwaka 2000, kulikuwa na mauaji ya Kanungu Uganda ambapo Joseph Kibwetere alihusika na mauaji ya zaidi wakristo 900.
Mwaka wa 1978, pia yaliwahi kutokea mauaji ya Jonestown huko Guyana ambapo kasisi Jim Jones aliwadanganya wafuasi wake waweze kujidunga sindano zenye sumu yaliyoegemea misimamo mibaya iliotokamana na itikadi za kihamasa.