Miili ya marehemu watano waliofariki kwenye ajali ya lori la Dangote lililogongana na gari ndogo kisha kuwaka moto, imehamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa na uchunguzi zaidi baada ya baadhi kushindwa kutambulika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema miili ya watu watatu waliokuwa kwenye Lori la Dangote haijaweza kutambulika mara moja kutokana na kuteketea kwa moto.

Aidha Kamanda Onesmo amesema chanzo cha ajali bado kinachunguzwa.

Endelea kufuatili Dar24Media kwa taarifa zaidi.

RC Makonda awashangaa Chadema, 'Akili ndogo haiwezi kujadili mambo makubwa'
Chameleone afunguka Harmonize kufuta sauti yake, ‘sipendi kukosewa heshima’