Kocha Mikel Arteta ametetea uamuzi wake wa kutomtoa, Jurrien Timber mapema katika ushindi wa mabao 2-1 ambao Arsenal ilipata dhidi ya Nottingham Forest baada ya Mholanzi huyo kupata jeraha la goti, juzi Jumamosi.
Pambano lake na Brennan Johnson katika kipindi cha kwanza lilimfanya Timber achechemee, lakini aliendelea hadi dakika ya 50 kabla ya kutolewa nje, huku mchezaji wa kimataifa wa Japan, Takehiro Tomiyasu, akichukua nafasi yake.
Baada ya mchezo huo, Arteta aliulizwa kama alipaswa kumtoa Timber mapema, lakini akasisita beki huyo aliruhusiwa kuendelea na madaktari.
“Madaktari walimtazama walifurahi kwa yeye kuendelea,” alisema bosi huyo wa Arsenal.
“Mara moja katika hatua ya kwanza ya kipindi cha pili alifanya harakati na ilikuwa ya kuchekesha. Tulimtoa nje moja kwa moja na sasa inabidi tumtathmini na kuona ana nini.”
Tomiyasu aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Timber, huku Arteta akiamua kutomwita beki wa kati wa Brazil, Gabriel Magalhaes, ambaye kwa mshangao alianzia kwenye benchi.
Arteta alithibitisha Gabriel hakuwa majeruhi na aliachwa tu kama uamuzi wa busara.
“Ndio, tulitarajia mchezo ambao ulifanyika na tulihitaji mtu mwingine katika safu ya kati kufanya kile tulichofanya vyema zaidi,” alisema.
Mchezaji mmoja wa kwanza ambaye alifurahia mechi bora ya kwanza ya ligi akiwa na rangi za Arsenal alikuwa kiungo, Declan Rice, ambaye alimvutia sana kocha wake.
“Umemwona juzi Jumamosi, sijui ilikuwa baada ya dakika mbili au baada ya kumi, lakini jinsi anavyosonga, jinsi anavyocheza na kujumuika kwenye chumba cha kubadilishia nguo nadhani anafurahia nafasi hiyo,” alieleza Arteta.
“Labda angefunga mabao mawili juzi Jumamosi, na alikuwa na furaha kubwa sana kwa kile alichokuwa akikifanya uwanjani.”